Kontardo wa Este
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kontardo wa Este (Ferrara, Italia, 1216 - Broni, Pavia, Italia, 16 Aprili 1249) alikuwa mwana wa mtemi wa Ferrara. Dada yake, Beatrice, alikuwa malkia wa Hungaria. Hata hivyo Kontardo alijinyima cheo na mali akaishi miaka mingi kwa ufukara mkubwa bila makao maalumu akatembelea patakatifu pa Yerusalemu, Palestina[1].

Baadaye, akielekea patakatifu pa Santiago de Compostela, Hispania, aliugua njiani na kufariki amelala juu ya nyasi nyumbani mwa mkulima akatambuliwa baadaye tu, kutokana na miujiza kadhaa iliyotokea [2].
Tangu kale anaheshimiwa kama watakatifu. Papa Paulo V alithibitisha heshima hiyo tarehe 27 Septemba 1628.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads