Uhindu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Uhindu
Remove ads

Uhindu (kwa Kisanskrit: हिन्दू धर्म: Hindū Dharma; pia सनातन धर्म Sanātana Dharma) ni dini kubwa yenye asili katika Bara Hindi.Ikiwa na wafuasi milioni 900 ni dini ya tatu baada ya Ukristo na Uislamu kwa wingi wa waumini.

Ukweli wa haraka
Remove ads

Nchi zenye Wahindu

Katika nchi za India, Nepal na Morisi na kwenye kisiwa cha Bali (Indonesia) wakazi wengi hufuata aina mojawapo ya Uhindu.

Vikundi vikubwa viko pia:

Remove ads

Jina

Neno Hindu linatokana na lugha ya Kisanskrit ambapo Sindhu ni jina la kale la mto Indus uliopo kwenye sehemu ya magharibi kaskazini ya Bara Hindi. "Hindu" imepatikana mara ya kwanza wakati wa karne ya 6 KK katika andishi la mfalme Darius I kwa maana ya "watu wa ng'ambo ya mto Indus (Kisanskrit: Sindhu).[3] Hapa "Sindhu / Hindu" haina maana ya kidini bali ya kijiografia pekee.

Katika Kiajemi neno "Hindu" linamaanisha wakazi wa Uhindi pamoja na wafuasi wa dini kubwa ya nchi hiyo. Mnamo karne ya 11 milki iliundwa na Waajemi katika Bara Hindi iliyoitwa "Hindustan" na mji mkuu ulikuwa Lahore[4].

Baadaye Waingereza walipokea jina hilo kutoka Kiajemi, wakilitumia kwanza kwa nchi na baadaye hasa kwa wafuasi wa dini zisizo za Kiislamu, Kiyahudi wala Kikristo. Jina Hinduism (iliyoandikwa mwanzoni Hindooism) lilikuwa kawaida tangu karne ya 18 kwa kutaja falsafa na dini zenye asili ya India.[5]

Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads