Morisi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Morisi
Remove ads

Morisi, rasmi kama Jamhuri ya Morisi, ni nchi ya kisiwa katika Bahari ya Hindi, mashariki mwa pwani ya bara la Afrika, takriban kilomita 2,000 kutoka pwani ya Afrika ya mashariki. Inajumuisha kisiwa kikuu cha "Morisi, Rodrigues, visiwa vidogo vya Cargados Carajos na Agalega" ambavyo ni sehemu ya funguvisiwa la Maskarena pamoja na kisiwa cha Réunion ambacho ni mkoa wa Ufaransa. Ina idadi ya watu takriban milioni 1.3, ikiwa ya 157 duniani. Jiji lake kubwa zaidi na mji mkuu ni Port Louis. Morisi imegawanyika katika wilaya 9. Inajulikana kwa mandhari yake ya kuvutia ya kitropiki na utalii wa pwani .

Ukweli wa haraka Jamhuri ya Morisi République de Maurice (Kifaransa) Repiblik Moris (Kimaorisi), Mji mkuu na mkubwa ...
Remove ads
Thumb
Ramani ya kisiwa cha Morisi

Morisi ina historia tajiri inayochanganya ushawishi wa Asia, Afrika na Ulaya. Kabla ya ukoloni, visiwa vya Morisi havikuwa na wakazi wa kudumu. Vilivumbuliwa na Wareno katika karne ya 16, na baadaye kutawaliwa na Wafaransa na Waingereza, kabla ya kupata uhuru mnamo mwaka 1968. Tangu hapo, Morisi imejijengea sifa kama mojawapo ya nchi thabiti zaidi kisiasa na kiuchumi barani Afrika, ikiwa na mfumo wa demokrasia wa kibunge na maendeleo ya kijamii yaliyopimika.

Lugha rasmi inayotumika katika bunge ni Kiingereza, ingawa Kifaransa na [[Krioli ya Kimorisi ndiyo zinazotumika zaidi katika maisha ya kila siku. Morisi ina jamii yenye mchanganyiko wa tamaduni, ikiwa na wakazi wa asili ya Uhindi, Afrika, Uchina na Ulaya. Dini kubwa ni Uhindu, Ukristo, Uislamu na Ubudha, na jamii mbalimbali huishi kwa amani na kuvumiliana. Uchumi wa nchi hii unategemea utalii, bidhaa za nguo, sukari, na huduma za kifedha.

Remove ads

Jiografia

Visiwa vya jamhuri vimesambaa katika eneo pana sana:

Kisiwa kikuu cha Mauritius ni km² 1,865 au 91% za ardhi yote ya jamhuri. Karibu wakazi wote (1,261,208) huishi huko.

Kisiwa cha Rodrigues kipo km 560 mashariki kwa Morisi yenyewe. Eneo lake ni km² 109; kuna wakazi 41,000.

Thumb
Visiwa vya Makarena kati ya visiwa vya Kiafrika katika Bahari Hindi

Visiwa vya Cargados Carajos (vinaitwa pia Saint Brandon) ni visiwa 16 vidogo sana, vyenye eneo la km² 1.3 pekee. Viko km 300 kaskazini kwa Morisi. Kuna wakazi mia chache wavuvi.

Agalega ni visiwa viwili, yaani Kisiwa cha Kaskazini na Kisiwa cha Kusini, takriban km 1,122 kaskazini kwa Morisi yenyewe. Visiwa hivyo vina eneo la km² 70. Kuna vijiji vya Vingt Cinq na La Fourche kwenye kisiwa cha kaskazini na kijiji cha Ste Rita kwenye kisiwa cha kusini. Wenyeji wanalima mazao ya mnazi pamoja na mboga kwa matumizi yao wenyewe.

Remove ads

Demografia

Watu wa Morisi ni mchanganyiko mkubwa kutokana na historia ya visiwa hivyo.

Baada ya Waarabu na Wareno kuvumbua Morisi, wakazi wa kwanza (1638) walikuwa Waholanzi, lakini hawakuacha dalili isipokuwa majina ya mahali kwa sababu waliondoka mwaka 1710 baada ya kushindwa kiuchumi.

Wafaransa walitawala visiwa kati ya 1715 hadi 1810. Walianzisha miji na mashamba ya miwa. Nje ya walowezi, Wafaransa walipeleka pia watumwa kutoka bara la Afrika. Mwaka 1767 walikuwepo Wafaransa 3,163 pamoja na watumwa Waafrika 15,000, pia Wahindi 587.

Uingereza ulichukua utawala wa visiwa mwaka 1810 katika vita dhidi ya Napoleon. Siku zile Kiingereza kilikuwa lugha rasmi ya serikali, lakini wakazi waliendelea kutumia lahaja za Kifaransa.

Baada ya kuwapatia watumwa uhuru, Waingereza walileta Wahindi wengi, baadaye pia Wachina kama wafanyakazi kwenye mashamba ya sukari. Leo hii idadi kubwa ya wakazi ni wa asili ya Uhindi (67%), wakifuatwa na Waafrika (28%), Wachina (3%) na Wafaransa (2%).

Lakini 90% ya wananchi hutumia krioli ya Kimorisyen (aina ya Kifaransa) kama lugha ya kwanza. Asilimia 5 hutumia Kibhojpuri au lugha za Uhindi kama vile Kiurdu, Kitamil. Asilimia 4.4 hutumia Kifaransa, na 0.6% tu Kiingereza.

Karibu nusu (47.9%) ya wakazi hufuata dini ya Uhindu, 32.3% Ukristo (hasa wa Kanisa Katoliki) na 18.2% ni Waislamu (hasa Wasunni, lakini pia Washia).

Remove ads

Uchumi

Hadi leo kilimo cha miwa (sukari) ni uti wa mgongo wa uchumi wa Morisi.

Nchi iliendelea kuwa na serikali zilizochaguliwa bila kupinduliwa: hali hii ya utulivu ilisaidia kukua kwa uchumi. Hali ya maisha ni ya juu kuliko nchi nyingi za Afrika.

Tazama pia


Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Morisi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads