Maria Goretti

From Wikipedia, the free encyclopedia

Maria Goretti
Remove ads

Maria Teresa Goretti (Corinaldo, Ancona, Italia, 16 Oktoba 1890 - Nettuno, Lazio, 6 Julai 1902) alikuwa bikira Mkristo ambaye, baada ya kupitia utoto katika ufukara akimsaidia mama yake mjane katika shughuli za nyumbani na kudumu katika sala, alikataa mfululizo kuzini na jirani yake Alessandro Serenelli, mpaka huyo akamchoma mara 14 mfululizo kwa kifaa cha chuma[1].

Thumb
Sanamu ya Mt. Maria Goretti katika mavazi ya mkulima akishika maua na kisu.
Thumb
Nyumba alimoishi na kupigwa Maria Goretti.

Akizidi kuchomwa, Maria alisisitiza msimamo wake: "Usifanye, ni dhambi!"

Kabla hajafa hospitalini, Maria alimsamehe muuaji wake kwa kumtakia awe naye mbinguni.

Baada ya miaka mitatu gerezani, Alessandro aliongoka na alipotoka alikwenda kuomba msamaha wa mama wa Maria, akakubaliwa kwa hoja kwamba, "Mwanangu amekusamehe wakati wa kufa, nami siwezi kufanya tofauti". Kesho yake walipokea ekaristi pamoja.

Halafu akaishi utawani kwa Wakapuchini wa Macerata hadi alipofariki mwaka 1970.

Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 27 Aprili 1947 na kuwa mtakatifu tarehe 24 Juni 1950, wakihudhuria mama yake na muuaji vilevile[2].

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe ya kifodini chake, 6 Julai ya kila mwaka[3].

Remove ads

Tazama pia

Filamu juu yake

  • Cielo sulla palude, kwa ajili ya sinema, iliongozwa na Augusto Genina, Italia 1949
  • Maria Goretti, kwa ajili ya televisheni, iliongozwa na Giulio Base, Italia 2002

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads