Mbwana Samatta

Mchezaji wa chama cha soka Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Mbwana Samatta
Remove ads

Mbwana Ally Samatta, (alizaliwa 23 Disemba 1992), ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Tanzania katika klabu ya Feberbahce nchini Uturuki [1]. Mbwana ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na kabla ya kuhamia klabu ya Feberbahce (Uturuki) alikuwa akucheze timu ya Aston Villa nchini Uingereza[2].

Ukweli wa haraka Maelezo binafsi, Jina kamili ...

Samatta alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya African Lyon F.C. mwaka 2008 nchini Tanzania. Alisajiliwa na klabu ya Simba mwaka 2010, ambapo alicheza katika nusu msimu tu kabla ya kujiunga na klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Alicheza kwa miaka mitano ndani ya TP Mazembe na kujijengea nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Mwaka 2015, alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka wa Afrika, na kumaliza msimu akiwa mfungaji bora wa mashindano ya klabu bingwa Afrika (Ligi ya Mabingwa Afrika) na kuisaidia klabu yake kushinda taji hilo.

Samatta alijiunga na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji mnamo januari 2016, aliisaidia kufuzu michuano ya Ulaya maarufu kama Europa Ligi na kushinda taji la ligi ya Ubelgiji (Belgian Jupiler Ligi mwaka 2019. Alimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo akashinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe award)[3].

Manamo Januari mwaka 2020, Samatta alisajiliwa na klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza na kuwa mchezaji wa kwanza kutoka nchini Tanzania kucheza na kufunga goli ligi kuu ya nchini Uingereza.

Remove ads

Kazi

Samatta alikua mchezaji muhimu wa TP Mazembe waliposhinda taji la klabu bingwa Afrika mwaka 2015 (2015 CAF Champions Ligi), akifunga jumla ya magoli saba na kumaliza akiwa mfungaji bora.[4]

Mnamo Januari 2016, aliposhinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutokea Afrika ya Mashariki kutwaa tuzo hiyo. Katika ugawaji wa tuzo hizo uliofanyika jijini Abuja, Nigeria, tarehe 7 Januari 2016, Samatta alikusanya jumla ya alama 127, akimzidi mchezaji mwenzake Robert Kidiaba mlinda lango wa TP Mazembe na timu ya taifa ya DR Congo aliyepata alama 88. Baghdad Bounedjah raia wa Algeria alishika nafasi ya tatu akiwa na alama 63.[5] Katika mchezo dhidi ya Moghreb Tétouan ya Moroko, Samatta alifunga magoli matatu kwa mpigo (hat-trick) yaliyowafanya wasonge hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika. Magoli hayo yanakumbukwa sana katika historia ya klabu ya TP Mazembe.[6]

Genk

Muda mfupi baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, alijiunga na klabu ya K.R.C. Genk kwa mkataba wa miaka minne na nusu.[7] Tarehe 23 Agosti 2018 Samatta alifunga goli tatu kwa mpigo(hat-trick) dhidi ya Brøndby IFkwenye mashindano ya Ulaya maarufu kwa jina la Europa Ligi walfanikiwa kupata ushindi wa goli 5–2.[8] Mei 2019 aliishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe).

Aston Villa

Mnamo Januari 20, 2020, Samatta alijiunga na klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi Kuu ya Uingereza kwa mkataba wa miaka minne na nusu.[9] Uhamisho huu ulimfanya Samatta kuwa mchezaji wa kwanza wa kitanzania kucheza ligi kuu ya Uingereza.[10] Ada ya uhamisho inakadiriwa kuwa £8.5 milioni.[11][12] Mchezo wa kwanza alicheza siku nane baada ya kusajiliwa dhidi ya Leceister City kwenye mzunguku wa pili wa mashindano ya Carabao hatua ya nusu fainali, waliibuka na ushindi wa magoli 2 – 1, kwa matoke ohayo, Villa walifika hatua ya fainali.[13]

Samatta alifunga goli lake la kwanza manamo 1 Februari 2020, walipocheza na Bournemouth, mchezo ulimalizika kwa Villa kushinda magoli 2 - 1. Goli hilo lilimfanya Samatta kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza na kufunga kwenye mashindano ya Ligi ya Uingereza.[14]

Fenerbahçe

Samatta alijiunga na Klabu ya Fernabahce ya nchini Uturuki tarehe 25 Septemba 2020, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.[15] Ulipofika mwisho wa mkopo mnamo Julai 2021, Samatta alisaini mkataba wa miaka minne, hii ilikua ni sehemu ya makubaliano ya uhamisho wake.[16]

Tarehe 1 Septemba 2021, Samatta alijiunga na Royal Antwerp ya nchini Ubelgiji kwa mkopo wa msimu mzima.[17]

Ilipofika 16 Agosti 2022, Samatta alirudi tena Genk kwa mkopo, uhamisho huo ulikua na chaguo la Genk kumnunua.[18]

PAOK

Mnamo tarehe 17 Julai 2023, timu ya nchini Ugiriki PAOK ilitangaza kumsajili Samatta kwa mkataba wa miaka miwili, mkataba huo ulikua na nafasi ya kuongeza mwaka mmoja.[19]


Remove ads

Maisha binafsi

Mbwana Samatta ni Mndengereko kutoka Kibiti kwa kabila. Katika maisha ya imani ni Muislamu.[20]

Takwimu za michezo

Klabu

Maelezo zaidi Klabu, Msimu ...

Kimataifa

[21]

Maelezo zaidi Mwaka, Michezo ...

Magoli Kimataifa

Maelezo zaidi Goli, Tarehe ...
Remove ads

Heshima

TP Mazembe[24]

  • Linafoot: 2011, 2012, 2013, 2013–14
  • DR Congo Super Cup: 2013, 2014
  • Klabu bingwa Afrika: Klabu bingwa Afrka 2015[25][26]

Genk

  • Ligi kuu ya Ubelgiji: msimu wa 2018–19[27]
  • Belgian Super Cup: michuano ya pili ya Ubelgiji 2019[28]

Binafsi

  • Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika: 2015
  • Timu yam waka ya CAF: 2015[29]
  • Mfungaji bora ligi ya mabingwa Afrika: 2015[4]
  • Mchezaji bora ligi ya Ubelgiji: 2019[3]
  • Mfungaji bora ligi ya Ubelgiji: msimu wa 2018-19[28]
Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads