Modesti wa Yerusalemu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Modesti wa Yerusalemu (Sivas, Kapadokia, leo nchini Uturuki, karne ya 6 – 17 Desemba 630[1]) alikuwa askofu wa mji huo nchini Israeli.

Kabla ya hapo aliuzwa kama mtumwa kwenda Misri. Huko alimuongoa bwana wake ambaye alimuacha huru. Hapo alijiunga na umonaki kwenye mlima Sinai. Baadaye akafanywa abati wa monasteri huko Palestina.
Mwaka 614 Kosroe II wa Persia aliteketeza Yerusalemu akiua Wakristo 66,509. Modesti alichaguliwa kushika nafasi ya askofu Zakaria aliyetekwa, na huyo alipofariki Modesti akawa askofu. Alijitahidi sana kujenga upya monasteri kadhaa hata zikajaa wamonaki na makanisa yaliyoteketezwa kwa moto [2][3].
Tangu kale ametambuliwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 17 Desemba[4] na nyinginezo.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads