New Jack Swing

From Wikipedia, the free encyclopedia

New Jack Swing
Remove ads

New Jack Swing ni mtindo wa muziki uliounganisha vipengele vya R&B, hip hop, na pop[1][2] ambao ulianza kupata umaarufu mwishoni mwa miaka ya 1980 hadi katikati ya miaka ya 1990. Mtindo huu ulitambulika kirahisi kwa midundo mizito, ala za elektroniki, na mapigo ya faafu yaliyochanganywa ala za hip hop na funk ndani ya mseto laini wa sauti za R&B. Mtindo huu wa muziki ulisaidia kuleta mabadiliko makubwa katika muziki wa R&B na pia kuwaweka wasanii Wamarekeni Weusi kuvuka ng'ambo ya kimataifa.[3]

Thumb
Teddy Riley katika Ziara ya 90's Block Party.

New Jack Swing ulibuniwa na Teddy Riley, mwanamuziki, mtayarishaji na mpiga ala anuwai kutoka Marekani. Riley hakuwa peke yake katika kuunda mkong'o sio wa muziki huu bali pamoja na mchango wa mtayarishaji maarufu Bernard Belle, Jimmy Jam and Terry Lewis.

Riley ndiye aliyefanya mtindo huu kuwa maarufu na mwenyewe alitengeneza nyimbo nyingi za New Jack Swing ambazo zilitamba sana. Hasa kuanzia miaka ya 1987 akiwa na kundi lake la Guy. Hawa walizalisha mtindo huu maarufu.[4]

Remove ads

Baadhi ya nyimbo na wasanii maarufu

Maelezo zaidi #, Wimbo ...
Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads