Odilo wa Cluny
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Odilo wa Cluny (962 hivi - 1 Januari 1049) alikuwa abati wa tano wa monasteri ya Kibenedikto ya Cluny nchini Ufaransa, ambaye aliifanya kuwa muhimu kuliko zote za Ulaya na kuhamasisha urekebisho wa nyingine nyingi.

Mkali kwake mwenyewe, alikuwa mpole na mwenye huruma kwa wengine; kwa jina la Mungu alipatanisha mataifa yaliyokuwa yanapigana, wakati wa njaa alitegemeza kwa hali na mali wanyonge. Pia alianzisha kumbukumbu ya Marehemu Wote siku iliyofuata sikukuu ya Watakatifu Wote[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads