Omdurman
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Omdurman (au: Omdourman, Kar: أم درمان Umm Durmān ) ni mji mkubwa kabisa nchini Sudan kando ya mto Nile ikitazama mji mkuu Khartoum. Pamoja na Khartoum na Bahri ni mji mmoja kubwa sana unaounganishwa na madaraja kadhaa.



Una wakazi wanaokadiriwa kufikia karibu milioni 3.
Remove ads
Historia
Mji ulianzishwa na Muhammad Ahmad ibn Abd Allah Al-Mahdi mwaka 1885. Baada ya jeshi lake kuteka Khartoum katika vita dhidi ya Misri na gavana yake Gordon Mahdi Muhammad hakutaka kukaa kwenye "mji wa makafiri" akajenga mji mpya wa Omdurman "mji wa waumini" ng'ambo ya mto Nile uliokuwa mji mkuu wa dola la Mahdi 1885 - 1898. Wakati ule Omdurman ilikuwa tayari na wakazi 150,000.
Waingereza walipoteka Sudan mwaka 1898 Omdurman ilirudi nyuma lakini wakati wa miaka ya mwisho wa karne ya 20 ilikua tena kupita Khartoum kutokana na kufika kwa wakimbizi wengi mjini kutoka nchi jirani kama Chad, Eritrea, Ethiopia na Uganda, pia wakimbizi kutoka vita ya Sudan ya Kusini. Wakimbizi hawa walijenga mitaa mikubwa ya vibanda.
Remove ads
Utamaduni na elimu
Omdurman ina vyuo vikuu kadhaa.
Kumbukumbu ya kihistoria muhimu ni kaburi la Mahdi.
Tazama pia
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Sudan bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Omdurman kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads