Nile

From Wikipedia, the free encyclopedia

Nile
Remove ads
Remove ads

Mto Nile (pia: Naili; kwa Kiarabu: ‏ ,النيل‎ an-nīl) ni mto mkubwa upande wa mashariki ya bara la Afrika. Mara nyingi hutajwa kuwa pia ni mto mrefu kabisa duniani kushinda mto Amazonas. Kutoka Ziwa la Viktoria Nyanza hadi mdomo wake kwenye Bahari ya Mediteranea Nile inavuka nchi za Uganda, Sudan Kusini, Sudan na Misri kwa urefu wa km 6,650.

Thumb
Mto Nile,Uganda
Maelezo zaidi Nchi za beseni la mto wa Nile pamoja na matawimto yake, Mto wa Nile ...
Thumb
Picha ya Nile kutoka chombo cha angani - (Shukrani kwa NASA).

Beseni la Nile hukusanya maji ya eneo linalojumlisha 10% za eneo la Afrika yote au km² 3,349,000. Takriban watu milioni 250 hukalia beseni hilo.

Remove ads

Jina

"Nile" au "Naili" ni umbo la Kiingereza la jina la mto lililotokana na lile lililotumiwa na Wagiriki wa Kale: "Neilos" (Νεῖλος). Haijulikani Wagiriki walipata jina hilo kwa njia gani, lakini lilikuwa kawaida nje ya Misri.

Wamisri wa Kale waliita mto huu kwa jina Ḥ'pī au Iteru linalomaanisha "mto mkubwa". Wakopti walikuwa na jina la piaro lakini tangu utawala wa Kiroma jina la Kigiriki lilizidi kutumika, na Waarabu waliendelea na jina la Kigiriki pia, hivyo leo hii wananchi wanasema "an-nil".

Remove ads

Chanzo cha Nile

Nile ina vyanzo viwili, yaani

Majina hayo ya "nyeupe" na "buluu" yana asili yake katika mji wa Khartoum ambako mito yote miwili inaunganika ilhali kila mmoja una rangi tofauti kutokana na udongo tofauti uliotia rangi yake kwenye maji hayo.

Vyanzo vya Nile ni mito yote inayopeleka maji kwenda Ziwa Viktoria Nyanza katika nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda na Kenya. Chanzo cha mbali kabisa ni mto wa Luvironza huko Burundi unaoingia katika mto Kagera na kufika Ziwa Viktoria Nyanza.

Mkono mwingine wa Nile unaanza Ethiopia ukiitwa Abbai au Nile ya Buluu: unatoka katika Ziwa Tana.

Hakuna mapatano kabisa Nile inaanzia wapi. Kawaida ya waandishi Waingereza ni kuhesabu kuanzia Ziwa Viktoria; waandishi wa mataifa mengine huwa wanaweza wakaita tayari mto Kagera kwa jina "Nile ya Kagera".

Remove ads

Majina ya Nile

Majina ya sehemu ya mto kuanzia Ziwa Viktoria hadi Khartoum ni kama yafuatayo:

  • Nile ya Albert kuanzia Ziwa Albert hadi mpaka wa Sudan Kusini
  • kwa sababu ya rangi wakati wa mvua yake kutokana na udongo katika maji jina linakuwa Bahr al-Abyad kuanzia Bahr al-Ghazal hadi Khartoum

Matumizi wa maji ya Nile

Tangu milenia kadhaa maji ya Nile yamekuwa msingi wa maisha yote nchini Misri na pia kwa sehemu kubwa ya nchi ya Sudan.

Katika miaka ya 1920 Uingereza kama mtawala mkoloni wa Sudan na Misri ulikuwa na majadiliano juu ya ugawaji wa maji ya mto na kufikia mapatano juu ya matumizi ya maji ya mto Nile ya 1929.

Hadi leo Misri inadai ya kwamba mapatanao yale yanakataa ujenzi wa malambo na kuanzishwa kwa miradi ya umwagiliaji inayotumia maji ya Nile bila kibali cha serikali yake. Hapa Misri inadai ya kwamba nchi zote zilizokuwa makoloni ya Uingereza wakati ule zinafungwa na mapatano ya mwaka 1929 na hizi ni pamoja na Sudan, Uganda, Kenya, Tanzania, halafu pia Ethiopia iliyopatana na Uingereza wakati ule. Nchi nyingine hazikubali madai hayo, ila majadiliano juu ya mapatano mapya ya ushirikiano katika beseni la Nile yanaendelea.

Remove ads

Tazama pia

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nile kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads