Papa Caio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Caio alikuwa Papa kuanzia tarehe 17 Desemba 283 hadi kifo chake tarehe 22 Aprili 296[1]. Alitokea Dalmatia, leo nchini Korasya[2].

Alimfuata Papa Eutychian akafuatwa na Papa Marcellinus.
Wakati wa Upapa wake, chokochoko dhidi ya Wakristo zilianza kuongezeka tena, ingawa waliweza kujenga makanisa na kupanua mashamba ya Mungu. Alidai muumini asipewe uaskofu bila kupitia kwanza daraja zote za chini[3]. Alikwepa dhuluma ya kaisari Dioklesyano, anayesemekana alikuwa na undugu naye.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Maandishi yake
- Opera Omnia kadiri ya Migne katika Patrologia Latina
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads