Papa Felix III

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Felix III
Remove ads

Papa Felix III alikuwa Papa kuanzia tarehe 13 Machi 483 hadi kifo chake tarehe 25 Februari/1 Machi 492[1]. Alitokea Roma, Italia, katika ukoo maarufu.

Thumb
Mt. Felisi III.

Alimfuata Papa Simplicio akafuatwa na Papa Gelasio I.

Uamuzi wake wa kwanza ulikuwa kukataa hati maarufu kama Henotikon kwa sababu haikusema wazi kwamba Yesu Kristo ana hali mbili, Umungu na utu [2]. Uamuzi huo ulisababisha farakano la Acacius wa Konstantinopoli.

Upande wa Afrika Kaskazini aliamua suala la Wakatoliki waliokubali kubatizwa tena na Waario ili kukwepa dhuluma ya watawala Wavandali[3]. Kufuatana na sinodi maalumu ya mwaka 487 aliwaandika maaskofu wa huko masharti ya kuwapokea upya kundini[4][5].

Kutokana na watoto aliowazaa katika ndoa yake kabla hajachaguliwa, walipatikana baadaye Papa Agapeto I (mjukuu) na Papa Gregori I (kitukuu)[6][7][8].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 1 Machi[9][10].

Remove ads

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads