Papa Gelasio I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Gelasio I
Remove ads

Papa Gelasio I alikuwa Papa kuanzia tarehe 1 Machi 492 hadi kifo chake tarehe 21 Novemba 496[1]. Alikuwa Papa wa tatu mwenye asili ya Afrika kaskazini.[2][3][4]

Thumb
Mt. Gelasius I.

Alimfuata Papa Felix III akafuatwa na Papa Anastasio II.

Maarufu kwa ujuzi na uadilifu, alidai utiifu kwake kutoka kwa Wakristo wa Magharibi na Mashariki vilevile na kutetea kwa nguvu imani sahihi hata kuchangia mabishano, ingawa alikuwa na mahusiano mazuri na watawala Waostrogoti waliokuwa Waario[5].

Akisukumwa na upendo wake mkubwa na mahitaji ya maskini, ili kuwasaidia yeye mwenyewe alifariki fukara sana [6].

Remove ads

Maandishi

Mwandishi mahiri[7], kati ya Mapapa wa karne za kwanza, ndiye aliyeandika zaidi.

Mwaka 494, aliandika barua Duo sunt kwa kaisari Anastasius I kuhusu mahusiano ya Kanisa na Dola; barua hiyo aliathiri siasa kwa karibu miaka elfu.[8] Ili kuzuia mamlaka ya kaisari isidhuru umoja wa Kanisa, alichambua kwa dhati sifa za mamlaka hiyo ya kidunia na za ile ya kiroho, akisisitiza haja ya kila upande kuwa huru.

Pia zimetufikia barua zake nyingine zaidi ya 100[9]. Maandishi mengine yalitajwa kuwa ya kwake ingawa si kweli; lengo lilikuwa kuyatia maanani zaidi.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 21 Novemba[10].

Remove ads

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads