Papa Innocent I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Innocent I alikuwa Papa kuanzia tarehe 22 Desemba 401 hadi kifo chake tarehe 12 Machi 417[1]. Alitokea Albano, Roma, Italia[2].

Jambo la pekee katika historia ya Kanisa[3], alimfuata Papa Anastasio I, aliyemzaa kabla ya kupewa upadrisho, akafuatwa na Papa Zosimus.
Aliimarisha mamlaka ya Kanisa la Roma kwa kuamua kesi nyingi za pande zote mbili za Kanisa[4], Mashariki na Magharibi[5]. Alimtetea Yohane Krisostomo, alimfariji Jeromu na kumkubali Augustino [6].
Alieneza[7] kanuni ya vitabu rasmi vya Biblia inayolingana na ile itakayopitishwa na Mtaguso wa Trento miaka elfu baadaye[8][9][10].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Maandishi yake
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads