Papa Martin I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Martin I
Remove ads
Remove ads

Papa Martin I alikuwa Papa kuanzia tarehe 5 Julai 649 hadi kifodini chake tarehe 16 Septemba 655[1]. Alitokea Todi, Umbria, Italia[2].

Thumb
Mt. Martino I.

Alimfuata Papa Theodor I akafuatwa na Papa Eugenio I.

Baada ya kuwa balozi wa Papa Theodori I huko Konstantinopoli, alichaguliwa kuwa mwandamizi wake bila kibali cha kaisari wa Dola la Roma Mashariki.

Kwa kuwa katika Mtaguso wa Laterano (649) na baada yake alipinga uzushi ulioungwa mkono na kaisari Konstans II, wa kwamba Yesu alikuwa na utashi wa Kimungu tu, bila ule wa kibinadamu, hatimaye katika kanisa kuu la Roma akakamatwa na kupelekwa Konstantinopoli kama mfungwa, halafu uhamishoni sehemu za Ukraina kusini, alipofariki baada ya miaka miwili ya mateso[3][4].

Ndiyo sababu tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 13 Aprili[5].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading content...

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Loading content...

Viungo vya nje

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads