Papa Theodor I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Theodor I
Remove ads

Papa Theodor I alikuwa Papa kuanzia tarehe 12 Oktoba/24 Novemba 642 hadi kifo chake tarehe 14 Mei 649[1]. Mzaliwa wa Yerusalemu (Israeli)[2] ambapo baba yake alipata kuwa askofu [3], alikimbilia Roma Waislamu walipoteka Nchi Takatifu[4].

Thumb
Papa Theodori I.

Alimfuata Papa Yohane IV akafuatwa na Papa Martin I.

Alipinga uzushi wa waliokanusha Yesu kuwa na utashi wa kibinadamu na kwa ajili hiyo aliandaa Mtaguso wa Laterano wa mwaka 649 akishirikiana na Maksimo Muungamadini.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 18 Mei.[5]

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads