Papa Pontian
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Pontian (kwa Kilatini Pontianus; alifariki Oktoba 235) alikuwa Papa kuanzia tarehe 21 Julai 230 hadi tarehe 28 Septemba 235[1][2], alipojiuzulu ili kuwezesha uchaguzi wa mwandamizi wake akiwa amepelekwa uhamishoni katika kisiwa cha Sardinia pamoja na antipapa Hipoliti wa Roma[3][4]. Alitokea Roma, Italia.

Alimfuata Papa Urbano I akafuatwa na Papa Anterus.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini, hasa tarehe 13 Agosti, pamoja na Hipoliti.[5][6][7].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads