Papa Celestino I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Celestino I alikuwa Papa kuanzia tarehe 10 Septemba 422 hadi kifo chake tarehe 24 Julai 432[1]. Alitokea Campania, Italia na baba yake aliitwa Priscus.

Alimfuata Papa Boniface I akafuatwa na Papa Sixtus III.
Akiwa na juhudi za kulinda na kupanua Kanisa, alianzisha uaskofu katika visiwa vya Britania akaunga mkono Mtaguso wa Efeso katika kumuita Bikira Maria "Mama wa Mungu" dhidi ya mafundisho ya Nestori[2].
Alipambana pia na uzushi wa Upelaji [3] na kupigania nidhamu[4][5] pamoja na kudhibiti farakano la Novatianus[6].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 27 Julai[7] lakini pia 6 Aprili au 8 Aprili.
Remove ads
Tazama pia
Maandishi yake
- Opera Omnia katika Patrologia Latina ya Migne pamoja na faharasa
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads