Papa Sixtus III
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Sixtus III alikuwa Papa kuanzia tarehe 31 Julai 432 hadi kifo chake tarehe 19 Agosti 440[1]. Alitokea Roma, Italia.

Alimfuata Papa Selestini I akafuatwa na Papa Leo I.
Chini yake makanisa mbalimbali yalijengwa mjini Roma, hasa basilika la Bikira Maria lililowekwa wakfu kwa Mama wa Mungu kadiri ya sifa aliyopewa na Mtaguso wa Efeso (431). Pia alijitahidi kupatanisha maaskofu wa Mashariki (Aleksandria na Antiokia) na kutetea mamlaka ya Kanisa la Roma juu ya Iliriko[2].
Rafiki wa Agostino wa Hippo[3], tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe ya kifo chake[4].
Remove ads
Tazama pia
Maandishi yake
- Opera Omnia kadiri ya toleo la Migne katika Patrologia Latina pamoja na faharasa
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads