Papa Vitalian

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Vitalian
Remove ads

Papa Vitalian alikuwa Papa kuanzia tarehe 30 Julai 657 hadi kifo chake tarehe 27 Januari 672[1]. Alitokea Segni, Lazio, Italia[2].

Thumb
Papa Vitalian.

Jina la baba yake lilikuwa Anastasius[3].

Alimfuata Papa Eugenio I akafuatwa na Papa Adeodato II.

Kama Papa Eugenio I alijaribu kurudisha uhusiano mzuri na Dola la Roma Mashariki na Patriarki wa Konstantinopoli kuhusu uzushi uliofundisha kwamba Yesu hakuwa na utashi wa kibinadamu, lakini suala lilieleweka tu baadaye, katika Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli (680-681) uliolaani uzushi huo.

Alifaulu kuimarisha uhusiano na Wakristo wa Uingereza [4] kupitia sinodi ya Whitby[5] na Theodoro wa Tarso[6].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Kanisa Katoliki linaadhimisha sikukuu yake tarehe 27 Januari[7], lakini Waorthodoksi tarehe 23 Julai.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads