Papa Zakaria
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Zakaria alikuwa Papa kuanzia tarehe 3 Desemba 741 hadi kifo chake tarehe 15 Machi 752[1]. Alitokea Ugiriki[2] au Santa Severina, Calabria, Italia, labda akiwa na asili ya Balkani.

Jina la baba yake lilikuwa Polichronios.
Alimfuata Papa Gregori III akafuatwa na Papa Stefano II[3].
Anasifiwa sana na wanahistoria mbalimbali kwa jinsi alivyokabili vizuri mazingira magumu na ya hatari[4], akiongoza familia ya Mungu kwa umakinifu na busara ya hali ya juu [5].
Alifaulu kupatana na Walombardi walioteka sehemu kubwa ya Italia[6] au kupunguza ukali wao, aliwaelekeza Wafaranki namna ya kutawala kwa haki na kumhimiza Pipino Mfupi kujifanya rasmi mfalme wao[7], alifanya makabila ya Kijerumani yawe na makanisa zaidi, aliunga mkono umisionari wa Bonifas huko Ujerumani[8], alidumisha umoja na Kanisa la Mashariki, alipinga sera ya kaisari Konstantino V dhidi ya picha takatifu[7], alidhibiti mwelekeo wa kutunga majina kwa malaika[9] na alikataza biashara ya watumwa mjini Roma akiwakomboa waliokwisha kuletwa[6][10][11].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Maandishi yake
- Barua na hati zake zilitolewa na Jacques Paul Migne katika Patrologia Latina lxxxix. p. 917–960.
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads