Perpetui wa Tours
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Perpetui wa Tours (alifariki Tours, leo nchini Ufaransa, 30 Desemba 490 BK) alikuwa askofu wa 6 wa mji huo kwa miaka 30 baada ya ndugu yake Eustoki wa Tours na kabla ya ndugu yake mwingine, Volusiano wa Tours.

Alijenga basilika la Mt. Martino na makanisa mengine mengi kwa heshima ya watakatifu pamoja na kurudisha jimboni mwake desturi ya kufunga chakula na kukesha [1].
Gregori wa Tours aliandika juu yake[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Desemba[3].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
