Posidi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Posidi
Remove ads

Posidi (kwa Kilatini: Possidius; aliishi karne ya 4 na ya 5) alikuwa Mberberi askofu wa Calama katika mkoa wa Numidia wa Dola la Roma (leo nchini Algeria)[1].

Thumb
Possidius alikuwa askofu wa Calama, Numidia. Haya ni magofu ya mji huo wa kale.

Tangu kale Kanisa Katoliki linamheshimu kama mtakatifu, likiadhimisha sikukuu yake tarehe 16 Mei[2].

Maisha

Rafiki wa Augustino wa Hippo kwa miaka 40 (Vita S. Augustini, xxxi), aliandika habari za kuaminika juu ya maisha yake pamoja na orodha ya vitabu alivyoviandika[3].

Akiwa padri katika monasteri ya Augustino (ibid., xii), alipofanywa askofu mnamo mwaka 397, alianzisha monasteri jimboni pia.

Alipambana na Wadonati hata mmojawao alijaribu kumuua. Hata hivyo yeye alidai wasiadhibiwe kwa kutozwa faini kubwa ("Vita", xii; Augustine, "Ep.", cv, 4; "Contra Crescon.", III, xlvi).

Mwaka 408 alinusurika tena kuuawa na Wapagani (Augustine, "Epp.", xc, xci, xciii).

Mwaka 409 aliteuliwa kwenda Italia pamoja na maaskofu wengine ili kuomba Kaisari awalinde Wakatoliki dhidi ya Wadonati, tena mwaka 411 aliteuliwa kuwa na mhadara na Wadonati.

Mwaka 416 alishiriki Mtaguso wa Milevi uliopinga Upelaji.

Wavandali walipovamia Afrika Kaskazini alikimbilia Hippo akashuhudia kifo cha Augustino (430).

Mwaka 437 anajulikana alikuwa bado hai, akiishi uhamishoni baada ya kufukuzwa na mfalme wa Wavandali Gaiseriko aliyekuwa Mwario.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads