Queen Darleen
Mwanamuziki wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mwanahawa Abdul Juma (amezaliwa tarehe 4 Novemba 1985) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania.
Queen alianza muziki mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambapo alishirikishwa na Dully Sykes katika wimbo wake wa Historia ya Kweli au maarufu Sharifa na Mtoto wa Geti Kali wa Inspector Haroun. Baada ya hapo, alijikita katika muziki wa kujitegemea na mwaka 2006 alitoa kibao chake cha Wajua Nakupenda, alichofanya na Ali Kiba, chini ya utayarishaji wa KGT na usimamizi wa DJ Guru Ramadhani. Mwaka 2012, Queen alishinda tuzo ya Kili kwa wimbo bora wa Ragga/Dancehall.[1]
Baada ya harakati za muda mrefu, hatimaye alisainiwa na lebo ya WCB Wasafi iliyo chini ya Diamond Platnumz ambaye ni ndugu yake wa damu kwa upande wa baba.[2] Akiwa na WCB ametoa wimbo wake wa kwanza ukijulikana kama Kijuso uliotoka rasmi tarehe 17 Februari mwaka 2017 aliofanya na Rayvanny.[3] Halafu takufilisi (tarehe 9 Novemba mwaka 2017[4]) na Touch (tarehe 22 Novemba mwaka 2017[5]). Vilevile alishiriki kuimba katika wimbo wa pamoja wa WCB Zilipendwa ulitoka tarehe 25 Agosti 2017.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads