Romualdo Abati

From Wikipedia, the free encyclopedia

Romualdo Abati
Remove ads

Mtakatifu Romualdo (Ravenna, Emilia-Romagna, 951 / 953 - karibu na Fabriano, Marche, 19 Juni 1027) alikuwa abati nchini Italia na mwanzilishi wa urekebisho wa Wabenedikto Wakamaldoli.

Thumb
Mchoro wa Guercino, San Romualdo, Ravenna.

Anaheshimiwa kama mtakatifu na Kanisa Katoliki kuanzia miaka 5 baada ya kufa, na hasa tangu mwaka 1595.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 19 Juni[1].

Maisha

Maisha yake yamesimuliwa na mfuasi wake Petro Damiani katika kitabu alichokiandika miaka 15 hivi baada ya kifo chake (1042).

Kitabu rasmi cha watakatifu wa Kanisa la Roma (Martirologium Romanum) kinamkumbuka hivi: "Mtakatifu Romualdo, mkaapweke na baba wa wamonaki Wakamaldoli, ambaye, akiwa na asili ya Ravenna, na kutamani kushika maisha na nidhamu ya wakaapweke, alizunguka Italia miaka mingi, akijenga monasteri ndogo na kuhimiza kokote wamonaki wafuate maisha ya Kiinjili, mpaka alipomaliza vizuri juhudi zake katika monasteri ya Val di Castro mkoani Marche". [2].

Remove ads

Sala yake

Yesu mpenzi, amani ya moyo wangu, hamu isiyosemeka, utamu na unono wa malaika na wa watakatifu!

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads