Stefano Harding
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Stefano Harding (Sherborne, Dorset, Uingereza, 1060 hivi - Citeaux, Ufaransa, 28 Machi 1134) alikuwa mmonaki[1], padri, mwanzilishi mmojawapo[2] na abati[3] wa urekebisho wa Citeaux wa shirika la Benedikto wa Nursia.
Alifika Cîteaux kutoka Molesme pamoja na wamonaki wengine, akaongoza monasteri hiyo na kuanzisha huko tabaka la mabradha.
Katika uongozi wake wa miaka 25 aliongeza monasteri 12 alizoziunganisha chini ya Mwandiko wa Upendo, ili kusiwe na ugomvi wowote kati ya wamonaki bali wote waishi kwa kufuata amri ya upendo, kanuni moja na desturi za kufanana. Ndiye aliyempokea utawani Bernardo wa Clairvaux na wenzake 30[4][5].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads