Thomas Garnet
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Thomas Garnet, S.J. (Southwark, 1575 hivi – Tyburn, 23 Juni 1608) alikuwa padri Mjesuiti kutoka Uingereza aliyeuawa kwa kuwa Mkatoliki chini ya mfalme James I[1].

Baada ya kusoma huko Ufaransa na Hispania, alipadrishwa akarudi Uingereza (1599) alipofanya utume kwa kificho miaka 6 hadi alipokamatwa kwa mara ya pili. Miezi baadaye alifukuzwa nchini kwa tishio la kuuawa akirudi tena.
Alipomaliza unovisi katika shirika huko Louvain, alitumwa Uingereza alipokamatwa wiki 6 tu baadaye akauawa kwa kukataa kiapo cha kumtii mfalme badala ya Papa[2].
Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenyeheri tarehe 15 Desemba 1929, na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu mfiadini tarehe 25 Oktoba 1970.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads