Henry VIII wa Uingereza
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Henry VIII (28 Juni 1491 – 28 Januari 1547) alikuwa mfalme wa Uingereza kuanzia tarehe 21 Aprili 1509 hadi kifo chake. Ni wa pili kutoka nasaba ya Tudor, akimfuata baba yake, Henry VII.

Maisha na matukio
Wake sita wa Henry VIII
(kufuatana na mwaka wa ndoa)
(kufuatana na mwaka wa ndoa)
Katarina wa Aragon
(1509–1533)
(1509–1533)
Anne Boleyn
(1533–1536)
(1533–1536)
Jane Seymour
(1536–1537)
(1536–1537)
Anne of Cleves
(1540)
(1540)
Catherine Howard
(1540–1542)
(1540–1542)
Catherine Parr
(1543–1547)
(1543–1547)
Henry anajulikana hasa kwa kuoa wanawake sita, mmoja baada ya mwingine, na hasa kwa juhudi zake za kubatilisha ndoa yake ya kwanza na Katerina wa Aragona zilizomfanya hatimaye atenganishe Kanisa la Uingereza na Papa, akijifanya mkuu wa Kanisa. Pamoja na kutengwa na Kanisa Katoliki kwa sababu hiyo, aliendelea kusadiki mafundisho yake.[1]
Katika masuala ya ndani, Henry alijulikana kwa kubadilisha sana katiba ya nchi, akizidisha mamlaka yake mwenyewe. Waliopinga walishutumiwa kama wasaliti na mara nyingi kuhukumiwa adhabu ya kifo, akiwemo waziri mkuu Thomas More.
Matumizi yake yalikuwa makubwa mno, kwa ajili ya fahari na vita, hivi kwamba pesa nyingi alizofaulu kujipatia kwa kuteka mali ya monasteri na kuzuia kodi iliyokuwa inalipwa awali kwa Papa, hazikumtosha kamwe.
Aliunganisha Uingereza na Wales akawa pia mfalme wa kwanza wa Uingereza kushika nafasi ya mfalme wa Ireland.
Mwanzoni wengi walipendezwa naye[2], lakini baadaye alizidi kunenepa, afya yake ilitetereka, na hata nafsi yake ilivurugika na kumfanya mzinzi, mkatili, mwoga.[3]
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads