Tongoni

From Wikipedia, the free encyclopedia

Tongoni
Remove ads

Tongoni ni kata iliyopo ndani ya eneo la Jiji la Tanga katika Mkoa wa Tanga, Tanzania, yenye Postikodi namba 21207.

Thumb
Magofu ya Tongoni, Kata ya Tongoni, Wilaya ya Tanga.

Kata ina ukubwa wa kilomita za mraba 44 (maili 17),[1] pia ina mwinuko wa wastani wa mita 30 (futi 98)[2].

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 6,103 [3]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,594 [4][5] waishio humo.

Tongoni iko takriban kilomita 14 upande wa kusini wa kitovu cha jiji kando ya barabara inayokwenda Pangani, ikitazama Bahari Hindi.

Remove ads

Magofu ya Tongoni

Katika kata hiyo yanapatikana magofu ya Tongoni, mji wa Waswahili enzi za mawe za kati. Mahali pa kihistoria jinsi inavyoonekana leo kuna msikiti na takriban makaburi 20.[6]

Takriban miaka 600 iliyopita kulikuwepo hapa mji wa Tangata (pia: Mtangata) iliyokuwa mahali muhimu pa biashara. Mahali pake kwenye mdomo mpana wa mto unaoishia hapa palileta nafasi salama ya kutia nanga kwa jahazi. Inasemekana ya kwamba nahodha Mreno Vasco da Gama alipumzika hapa kidogo wakati wa safari yake ya kwanza kuelekea Bara Hindi mnamo mwaka 1498. Magofu ni pamoja na msikiti na makaburi yenye nguzo jinsi ilivyokuwa kawaida kwenye makaburi ya Waswahili.[7]

Picha

Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Vitabu

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads