Trafiki

From Wikipedia, the free encyclopedia

Trafiki
Remove ads

Trafiki ni jumla ya watumiaji wa njia za usafiri, hasa barabara, kama vile magari, mabasi, malori, waenda kwa miguu na mikokoteni. Ni pia jina la askari maalumu anayesimamia usalama barabarani[1]. Mtandaoni, neno trafiki lina maana ya idadi ya watumiaji wanaotembelea tovuti.

Thumb
Trafiki Gwalior, India

Matumizi

Nchini Kenya neno "trafiki" hutumika kumaanisha jumla ya watumiaji wa njia ya usafiri. Kwa mfano, Idara ya Trafiki ya polisi, sheria za trafiki na maafisa au polisi wa trafiki[2].

Nchini Tanzania, neno "trafiki" hutumika kama kuwa rejelea askari wa usalama barabarani[3].

Sheria za trafiki

Sheria za trafiki au pia sheria za barabarani ni sheria na taratibu zinazofuatwa ili kudumisha usalama kwa manufaa ya watumiaji wote wa barabara. Sheria msingi za barabarani zimeelezwa katika mkataba wa kimataifa, Mkataba wa Vienna wa Trafiki Barabarani wa mwaka 1968 ulio chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa. Kimsingi, mataa ya trafiki yanafaa kuzingatiwa, waenda kwa mguu wanafaa kupatia magari njia isipokuwa katika kivuko cha milia, waenda kwa mguu wanafaa kuwa makini wanapovuka barabara na magari yanafaa kutumia upande wa kuendeshea kulingana na sheria za nchi.

Kila nchi ina sheria msingi za barabarani. Serikali za mashinani kama zile za miji na kaunti zinaweza kuongezea kulingana na mahitaji yake. Sheria ya trafiki ya Kenya (kwa Kiingereza: Traffic Act Ilihifadhiwa 13 Julai 2019 kwenye Wayback Machine.) ndiyo sheria kuu ya barabarani.

Remove ads

Msongamano wa magari

Thumb
Basi la Mwendokasi (BRT) jijini Dar es Salaam.

Msongamano wa magari ni hali inayotokea wakati kuna magari mengi barabarani na kufanya mwendo wa magari kuwa wa polepole au kukoma. Majiji makubwa kama vile Nairobi na Dar es Salaam huathirika na hali hiyo hasa nyakati za asubuhi na jioni. Hali hii huathiri sana uchumi. Jiji la Dar es Salaam limejaribu kusuluhisha tatizo hili kwa kujenga mfumo wa mabasi ya mwendokasi[4].

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads