Verano wa Vence

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Verano wa Vence (alifariki 480 hivi) alikuwa askofu wa 4 wa mji huo wa Gaul (leo Ufaransa).

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Novemba[1].

Maisha

Kisha kufiwa mama yake Galla, alitawa pamoja na baba yake, Eukeri wa Lyon, na ndugu yake Saloni katika monasteri ya Lérins, iliyoanzishwa na Honorati wa Arles juu ya kisiwa karibu na Antibes[2].

Kutokana na sifa yake, baba yake alichaguliwa kuwa askofu wa Lyon mwaka 434 hivi akaendelea na cheo hicho hadi kifo chake.

Hapo Verano alishika nafasi yake[3] , na Saloni akawa askofu wa Geneva.

Verano alimuandikia Papa Leo I kumshukuru kwa jinsi alivyotetea imani sahihi kuhusu Neno alivyofanyika mtu katika barua kwa Flaviano wa Kostantinopoli [4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads