Waklara Fukara wa Kuabudu Mfululizo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Waklara Fukara wa Kuabudu Mfululizo (kwa Kilatini: Ordo Monialium Clarissarum a Perpetua Adoratione) ni tawi la shirika la kimonaki la Waklara lililoanzishwa na Maria Klara Bouillevaux (1820-1871) huko Paris, Ufaransa, mwaka 1854, likifuata kanuni ya Utawa Hasa III na katiba maalumu, yenye jambo la pekee la kuabudu ekaristi saa zote za usiku na mchana [1].

Mwaka 1912 monasteri zake zote zikapokea kanuni ya Urbani IV na kujiita Waklara Fukara wa Kuabudu Mfululizo. Walienea sana na kudumisha uhusiano na Wakapuchini. Hata katika nchi nyingine monasteri mpya ziliundwa na nyingine zilifunguliwa tena. Baadhi ziligeuka kuwa mashirika ya kitume, bila kuacha kanuni ya Kiklara.

Mwaka 2024 walikuwa na monasteri 39 walipoishi masista 493 [2].

Maarufu zaidi katika milenia mpya ni Maria Anjelika wa Kupashwa Habari (1923-2016) ambaye, karibu na monasteri yake ya kuabudu ekaristi mfululizo, alianzisha (1981) mtandao wa Kikatoliki mkubwa kuliko yote ya Amerika (EWTN)!

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads