Yosefu Cafasso
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yosefu Cafasso (kwa Kiitalia Giuseppe Cafasso; 15 Januari 1811 - 23 Juni 1860) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mwanaharakati kutoka Piemonte, Italia.
Pamoja na watakatifu Yosefu Benedikto Cottolengo, Yohane Bosco, Maria Dominika Mazzarello na Leonardo Murialdo aliwajibika kukabili matatizo ya jamii katika mji mkuu wa ufalme wa Sardinia, Torino. Hasa alishughulikia wafungwa na waliohukumiwa kufa ili kuwapatanisha na Mungu.
Pia aliwajibika kwa malezi ya kielimu na ya kiroho ya wenye wito wa upadri[1]
Cafasso alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri mwaka 1925, halafu na Papa Pius XII kuwa mtakatifu mwaka 1947.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads