Zuchu
Mwanamuziki na mwandishi wa nyimbo asili yake ni raia wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Zuhura Othman Soud (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii Zuchu; alizaliwa tarehe 22 Novemba mwaka 1993[1]) ni mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo na msanii wa kurekodi wa Kitanzania aliezaliwa Zanzibar. Ni mhamasishaji na muendelezaji nzuri wa mtindo mpya wa muziki unaoitwa Singeli. Nyimbo yake ya 'Hujanizidi' inadhihirisha jambo hili. Nyimbo zake nyingi ziko kwenye mtindo wa Singeli. Hivyo basi, tunaweza kumuita ni Malkia wa Singeli. Amesainiwa chini ya lebo ya WCB Wasafi Records chini ya uongozi wa Diamond Platnumz. [2] [3][4]
Alitunukiwa tuzo ya silver play button na mtandao wa kijamii wa Youtube kwa kuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika ya mashariki kwa kufikisha wafuasi zaidi ya 100,000 ndani ya wiki moja.[5]
Katika wiki ya kusheherekea siku ya kuzaliwa, Zuchu alitunukiwa tuzo ya msanii bora chipukizi wa mwaka 2020 na tuzo All Africa Music Awards AFRIMMA.[6]
Remove ads
Maisha ya awali
Zuchu amezaliwa kwenye familia ya wanamuziki. Ni binti wa mwanamuziki wa taarabu anayefahamika kwa jina la Khadija Kopa.[7][8][9][10] Zuchu alianza kuimba akiwa na umri mdogo na baadae kushirikiana na mama yake Khadija Kopa katika wimbo unaofahamika kama Mauzauza [11]
Zuchu alitambulika rasmi kwenye Tasnia ya muziki mnamo Aprili 2020. [12] Mpaka sasa ana albamu moja na alichaguliwa kushiriki mashindano ya kuwania tuzo ya MTV, MAMA awards ya mwaka 2021. Kwenye mashindano hayo, Zuchu alipangwa katika kipengele cha 'best breakthrough act', akikabiliana na ushindani kutoka kwa Elaine na Focalistic wa Afrika Kusini na Tems na Omah Lay wote kutoka Nigeria, John Blaq (Uganda) na Sha Sha (Zimbabwe). Mpaka sasa ana albamu moja na alichaguliwa kushiriki mashindano ya kuwania tuzo ya MTV, MAMA awards ya mwaka 2021. Kwenye mashindano hayo, Zuchu amepangwa katika kipengele cha 'best breakthrough act', anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Elaine na Focalistic wa Afrika Kusini na Tems na Omah Lay wote kutoka Nigeria, John Blaq (Uganda) na Sha Sha (Zimbabwe).[13]
Remove ads
Diskografia
Albamu
Zuchu aliachia albamu ya kwanza iliyotambulika kama “I am Zuchu“ mwaka 2020 ikiwa na nyimbo 7. [14] Albamu yake ndiyo iliyosikilizwa na watu wengi zaidi nchini Tanzania kwa mwaka 2020 na video za nyimbo zake zimetazamwa na mamilioni ya watu. Mwanamziku Zuchu kwasasa anatamba na albamu yake mpya hiitwayo Peace And Money yenye nyimbo kama Till I Die akiwa ame mshirikisha Spyro, Lollipop akiwa amemshirikisha Yemi Alade, Mwizi, Antenna, Makonzi, Lullaby akiwana Majeeed, I Don't Care, Mama, Nimechoka akiwa amemshirikisha msani mkubwa Tanzania Diamond. [15]
Remove ads
Nyimbo zake
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads