From Wikipedia, the free encyclopedia
Grasyano (kwa Kilatini: Catianus, Gatianus, Gratianus; kwa Kifaransa: Cassien, Gatien, Gratien)[1] (karne ya 3 BK) alikuwa askofu wa kwanza wa Tours (Ufaransa).
Kadiri ya wanahistoria Wakristo[2]. chini ya kaisari Decius (250 BK), Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia (Ufaransa wa leo) wakahubiri Injili: Grasyano huko Tours, Trofimo huko Arles, Paulo huko Narbonne, Saturnini huko Toulouse, Denis huko Paris, Austremoni huko Clermont na Martial huko Limoges.
Grasyano aliinjilisha kwa nusu karne dhidi ya upinzani wa wenyeji. Hata hivyo, kadiri ya Catholic Encyclopedia, alifaulu kukusanya waamini na kuwatuma kuanzisha makanisa, hivi kwamba alipofariki jimbo la Tours lilikuwa imara.
Baada ya kifo cha Grasyano, dhuluma dhidi ya Wakristo zilianza tena, hivyo jimbo lilibaki bila askofu kwa muda wa miaka 36, waamini walitawanywa kiasi cha kupoteza uhusiano na kazi ya mwanzilishi. Gregori wa Tours aliandika kwamba[3] askofu wa pili aliitwa Lidorius na kudumu miaka 33, mpaka alipofika Martino wa Tours mwaka 371.
Martino alikuta Wakristo wachache mjini, lakini kumbukumbu ya Grasyano ilikuwa hai. Martino mwenyewe aliona kaburi la Grasyano na kumheshimu daima.
Tangu kale Grasyano anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Desemba[4].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.