département ya Ufaransa From Wikipedia, the free encyclopedia
Guyani ya Kifaransa (kwa Kifaransa: Guyane française au Guyane tu, kwa Krioli ya Guyani ya Kifaransa Lagwiyann) ni eneo la ng'ambo la Ufaransa ("département d'outre-mer" au DOM) katika Amerika Kusini. Makao makuu ya Guyana ni mji wa Kayeni.
Guyane Lagwiyann | |
---|---|
Jina la Kifaransa | Guyane (kwa Krioli:Lagwiyann) |
Jina la kawaida | Guyani ya Kifaransa |
Mji Mkuu | Kayeni |
Eneo | 86 504 km² |
Mkuu wa Mkoa | Gabriel Serville |
Idadi ya wakazi | 301 099 |
Sensa ya mwaka | 2022 |
Wakazi kwa km² | 3.2 |
Wilaya (arrondissements) | 3 |
Ramani | |
Imepakana na Brazil na Surinam. Pwani ya Bahari ya Karibi (Atlantiki) iko upande wa kaskazini.
Eneo la Guyani ni mojawapo ya mikoa tisa ya nje zaidi (OR) ya Umoja wa Ulaya. Ni eneo pekee la bara la Ufaransa na Umoja wa Ulaya huko Amerika Kusini na eneo la mwisho la Ufaransa katika bara la Amerika.
Ilikuwa koloni la Ufaransa; sasa imekuwa sehemu kamili ya Ufaransa kisiasa na kisheria. Wakazi ni raia wa Ufaransa. Eneo lina hali ya mkoa (fr:département) na pia kanda (fr:région) katika Ufaransa. Hivyo Guyani ni sehemu ya Umoja wa Ulaya. Pesa yake ni Euro.
Idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa 296,711 katika mwaka 2019 na inaendelea kuongezeka kwa uzazi na uhamiaji.
Wakazi walio wengi ni wa asili ya Afrika au machotara wa mchanganyiko wa Kiafrika-Kizungu (Wakrioli) (60-70%). Asilimia 14 ni Wazungu, hasa kutoka Ufaransa; wengine ni Waindio asilia (3-4%), Wachina (3-4%), Wahindi na wahamiaji wa hivi karibuni kutoka Laos (1-2%), Vietnam, Lebanoni n.k.
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kifaransa.
Upande wa dini, wakazi walio wengi ni Wakristo wa Kanisa Katoliki (66.7%).
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini |
Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela |
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Guyani ya Kifaransa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.