Bernardino wa Siena
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Bernardino wa Siena (8 Septemba 1380 - 20 Mei 1444) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na kasisi wa Kanisa Katoliki.


Maisha ya awali

Alizaliwa na kubatizwa Massa Marittima (Siena) tarehe 8 Septemba 1380 katika familia Albizzeschi kutoka Siena, ambako alihamia baada ya kubaki yatima, ili alelewe na kusomeshwa na ndugu zake.
Wito na utume
Akiwa na umri wa miaka 22, alijiunga na utawa, katika tawi la urekebisho wa Waoservanti, ambalo akawa nguzo yake kuu, pamoja na Yohane wa Kapestrano, Yakobo wa Marka na Alberto wa Sarteano.
Kisha akaanza utume mkubwa akihubiri kwa mafanikio katika miji na vijiji vya Italia akivuta umati kwa maneno na mifano yake.
Kazi yake iliamsha katika Kanisa imani na ibada kwa Jina la Yesu na kurekebisha maadili ya wengi. Ndiye aliyesambaza kila mahali vibao vyenye kifupisho JHS (Jesus Hominum Salvator) kikiwa na msalaba juu yake na kuzungukwa na jua lenye miali 12[1].
Remove ads
Kifo
Alifariki huko L'Aquila, tarehe 20 Mei 1444.
Heshima baada ya kifo
Kutokana na sifa yake kubwa, alitangazwa mtakatifu na Papa Nikolasi V mwaka 1450.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads