Bikira Maria wa Rozari

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bikira Maria wa Rozari
Remove ads

Bikira Maria wa Rozari ni jina mojawapo linalotumika kwa Bikira Maria kuhusiana na rozari yake inayotumika kutafakari chini yake mafumbo ya Kristo, na kuomba ulinzi wa Mama wa Mungu, aliyeshiriki kwa namna ya pekee umwilisho, mateso na ufufuko wa Mwana wa Mungu kadiri ya imani ya Wakristo[1].

Thumb
Mafumbo 15 ya msingi ya Rozari na Bikira Maria wa Rozari.
Thumb
Njozi ya Mt. Dominiko, ilivyochorwa na Bernardo Cavallino, 1640 hivi.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 7 Oktoba[2], siku ambayo mwaka 1571 jeshi la majini la Wakristo lilifaulu kushinda lile la Waturuki Waislamu katika mapigano ya Lepanto, karibu na Ugiriki.

Ushindi huo haukutarajiwa, ila uliombwa na Wakatoliki wa Ulaya nzima kwa Rozari, kama alivyoagiza Papa Pius V[3][4]. Mjini Roma mwenyewe aliongoza maandamano ya ibada kwa ajili hiyo.

Matokeo yake yakawa ya kudumu: Waturuki hawakuweza kuteka Ulaya magharibi[5] wala kwenda Amerika kupitia bahari ya Atlantiki.

Basi, Papa alianzisha sikukuu ya kila mwaka kusherehekea ushindi huo.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads