Donulus

From Wikipedia, the free encyclopedia

Donulus
Remove ads

Donulus Rinaldi alikuwa mmojawapo kati ya wenzi wa Danieli Fasanella waliofia dini ya Ukristo huko Ceuta (Afrika Kaskazini) tarehe 10 Oktoba 1227. Walikuwa Ndugu Wadogo wamisionari huko Moroko.[1] Wote walikuwa mapadri isipokuwa Donulus.

Thumb
Kifodini cha Danieli na wenzake.

Walitangazwa watakatifu na Papa Leo X tarehe 22 Januari 1516.

Sikukuu yao inaadhimishwa kila tarehe 10 Oktoba[2][3].

Historia

Kifodini cha Berardo wa Carbio na wenzake kilichotokea Moroko mwaka 1219 kilifanya Wafransisko wengi watamani kufuata nyayo zao kwa kuhubiri Injili kwa wasio Wakristo.

Basi, mwaka 1227, uilofuata ule wa kifo cha mwanzilishi, Fransisko wa Asizi, watawa 6 wa kanda ya Toscana, Agnelus, Samueli, Donulus mwenyewe, Leo, Hugolino na Nikola wa Sassoferrato, walimuomba Elia wa Cortona, mkuu wa shirika, awaruhusu kwenda Moroko kuwahubiria Waislamu.

Kisha kukubaliwa, walikwenda Hispania, alipojiunga nao kama kiongozi Danieli Fasanella wa Belvedere, mkuu wa kanda ya Calabria.

Toka huko walivuka bahari ya Kati na tarehe 20 Septemba walishukia Afrika, walipobaki siku chache katika kijiji kilichokaliwa hasa na wafanyabiashara Wakristo.

Halafu, Jumapili asubuhi, waliingia mjini Ceuta, wakaanza mara kuhubiri kwa kupinga Uislamu. Kwa sababu hiyo walipekelekwa kwa sultani ambaye, akiwadhani ni vichaa, aliagiza watiwe gerezani. Walibaki humo hadi Jumapili iliyofuata, ambapo sultani kwa mabembelezo na vitisho alijaribu kuwafanya wakane dini yao.

Aliposhindwa, aliagiza wauawe. Kila mmojawao alimkaribia Danieli ili kupata baraka yake na ruhusa ya kumfia Yesu. Wote walikatwa kichwa [4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads