Samueli mfiadini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Samueli Iannitelli alikuwa mmojawapo kati ya wenzi wa Danieli Fasanella waliofia dini huko Ceuta tarehe 10 Oktoba 1227. Walikuwa Ndugu Wadogo wamisionari huko Moroko.[1] Wote walikuwa mapadri isipokuwa Donulus.

Walitangazwa watakatifu na Papa Leo X tarehe 22 Januari 1516.
Historia
Kifodini cha Berardo wa Carbio na wenzake kilichotokea Moroko mwaka 1219 kilifanya Wafransisko wengi watamani kufuata nyayo zao kwa kuhubiri Injili kwa wasio Wakristo.
Basi, mwaka 1227, uilofuata ule wa kifo cha mwanzilishi, Fransisko wa Asizi, watawa 6 wa kanda ya Toscana, Agnelus, Samueli mwenyewe, Donulus, Leo, Hugolino na Nikola wa Sassoferrato, walimuomba Elia wa Cortona, mkuu wa shirika, awaruhusu kwenda Moroko kuwahubiria Waislamu.
Kisha kukubaliwa, walikwenda Hispania, alipojiunga nao kama kiongozi Danieli, mkuu wa kanda ya Calabria.
Toka huko walivuka bahari na tarehe 20 Septemba walishukia Afrika, walipobaki siku chache katika kijiji kilichokaliwa hasa na wafanyabiashara Wakristo.
Halafu, Jumapili asubuhi, waliingia mjini Ceuta, wakaanza mara kuhubiri kwa kupinga Uislamu. Kwa sababu hiyo walipelekwa kwa sultani ambaye, akiwadhani ni vichaa, aliagiza watiwe gerezani. Walibaki humo hadi Jumapili iliyofuata, ambapo sultani kwa mabembelezo na vitisho alijaribu kuwafanya wakane dini yao.
Aliposhindwa, aliagiza wauawe. Kila mmojawao alimkaribia Danieli ili kupata baraka yake na ruhusa ya kumfia Yesu. Wote walikatwa kichwa [4].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads