Egesipo

Mtakatifu Mkristo wa karne ya 2 na mwandishi wa historia From Wikipedia, the free encyclopedia

Egesipo
Remove ads

Egesipo (110 hivi – Yerusalemu, Israeli/Palestina, 180) alikuwa Myahudi aliyeongokea Ukristo akawa mwandishi wa vitabu mbalimbali ambavyo sehemu chache tu zimetufikia[1][2]. Muhimu zaidi ni masimulizi yake manyofu juu ya historia ya Kanisa kuanzia Mateso ya Yesu hadi wakati alipoishi mwenyewe, lakini aliandika pia dhidi ya uzushi.

Thumb
Mt. Egesipo alivyochorwa.

Mwenyeji wa Mashariki ya Kati, aliishi miaka ishirini huko Roma chini ya Mapapa Aniseti, Soteri na Eleuteri [3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Aprili[4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads