Galdino wa Sala
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Galdino wa Sala (1096 hivi [1] – 18 Aprili 1176) alikuwa kardinali tena askofu mkuu wa Milano, Italia Kaskazini, miaka 1166-1176.[2]

Kwa nguvu zote aliunga mkono juhudi za Papa Alexander III, za Milano na za miji mingine ya Lombardia, dhidi ya Antipapa Victor IV (1159–1164) aliyetegemezwa na kaisari Frederick I Barbarossa.
Alihamasisha matengenezo ya mji ulioharibiwa na vita vya kupigania mamlaka.
Anakumbukwa pia kwa ukarimu wake kwa mafukara na kwa waliofungwa kutokana na madeni.
Alifariki baada ya kutoa hotuba dhidi ya wazushi.
Papa Alexander III mwenyewe alimtangaza mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads