George Washington
Rais wa kwanza wa Marekani From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
George Washington (22 Februari 1732 - 14 Desemba 1799) alikuwa mwanasiasa, kiongozi wa kijeshi na rais wa kwanza wa Marekani kati ya 1789 na 1797.





Remove ads
Maisha ya Awali
George Washington alizaliwa tarehe 22 Februari, 1732, katika Kaunti ya Westmoreland, Virginia, kwa wazazi Augustine na Mary Ball Washington. Alikuwa mtoto wa kwanza wa ndoa ya pili ya baba yake na alikulia kwenye mashamba kadhaa huko Virginia wakati wa ukoloni. Maisha yake ya awali yaliathiriwa na maadili ya tabaka la juu la Waingereza wa kikoloni—kufanya kazi kwa bidii, kumiliki ardhi, na uaminifu kwa Mfalme. Baba yake alipofariki mwaka 1743, George alirithi shamba la Ferry karibu na Fredericksburg, lakini kaka yake mkubwa wa kambo, Lawrence Washington, alipokea shamba maarufu zaidi la familia, Mount Vernon.
Washington alipata elimu ya msingi tu, hasa kutokana na matatizo ya kifedha baada ya kifo cha baba yake. Alisomea masomo ya vitendo kama hisabati, jiografia, na upimaji wa ardhi, ambayo baadaye yalimsaidia kupata kazi ya upimaji wa ardhi akiwa kijana. Akiwa na umri wa miaka 16, alijiunga na msafara wa kupima ardhi katika maeneo ya magharibi ya Virginia, ambapo alipata uzoefu na kuelewa maisha ya mipakani. Kazi hii ilimfanya akutane na watu wenye ushawishi na ikazidisha hamu yake ya kumiliki ardhi na kupanua maeneo.
Maisha ya awali ya Washington pia yaliathiriwa na tamaa ya kijeshi na hisia ya kuwajibika. Akiungwa mkono na kaka yake wa kambo Lawrence, ambaye alihudumu katika jeshi la Uingereza, George alipata nafasi ya kuwa mpimaji rasmi wa Kaunti ya Culpeper akiwa na umri wa miaka 17. Baada ya kifo cha Lawrence, George alikodisha shamba la Mount Vernon na kuanza kulitunza. Uzoefu huu wa awali uliweka msingi wa uongozi wake wa baadaye katika masuala ya kijeshi, kisiasa, na ya kiraia.
Remove ads
Mkulima na kiongozi wa kijeshi
Baada ya kifo cha kaka yake alirithi shamba kubwa pamoja na watumwa, akawa mkulima tajiri. Sehemu ya urithi ilikuwa cheo cha msimamizi wa wanamgambo waliokuwa kikosi cha kijeshi cha hiari waliotakiwa kusaidiana na wanajeshi Waingereza kutetea koloni dhidi ya majirani Waindio na Wafaransa walioenea kuelekea kusini kutoka koloni lao la Kanada - Quebec.
Katika umri mdogo wa miaka 22 Washington alijikuta kama mkuu wa wanamgambo katika vita vya Uingereza dhidi ya Wafaransa na Waindio vilivyopanuka baadaye kuwa Vita ya Miaka Saba. Akaongoza kikosi chake dhidi ya maadui akafaulu mara kadhaa.
Baadaye alishirikiana na jeshi rasmi la Uingereza katika mapigano ya Monongahela na kuongoza mabaki ya jeshi baada ya kifo cha jemadari Mwingereza. Mwaka 1755 akawa mkuu wa jeshi la koloni la Virginia. Lakini baada ya ushindi Waingereza walikataa kumpa cheo katika jeshi la mfalme, hivyo akajiuzulu akarudi kwenye shamba lake na kufuata siasa kwenye bunge la koloni.
Mwaka 1759 Washington akaoa mjane tajiri akawa kati ya matajiri wakuu kabisa wa Virginia.
Remove ads
Mapinduzi
Baada ya vita ya miaka saba uhusiano kati ya Uingereza na walowezi Waingereza katika makoloni yake 13 ya Amerika ya Kaskazini ukazorota. Tangu mwaka 1773 Waingereza walitumia sheria ya dharura na nguvu ya kijeshi mjini Boston. Wawakilishi wa makoloni yote 13 wakakutana kama bunge la Amerika Bara na Washington alikuwa miongoni mwao.
Baada ya mapigano ya kwanza kati ya wanajeshi Waingereza na wanamgambo wa walowezi, bunge likaamua kuunda jeshi la pamoja la makoloni yote na Washington akateuliwa kuwa jemadari mkuu.
Aliongoza jeshi la Marekani katika vita ya uhuru wa Marekani dhidi ya Uingereza hadi mwaka 1783.
Baada ya vita: mwanasiasa na rais
Baada ya uhuru wa Marekani George Washington akarudi kwake akalima tena lakini akachaguliwa pia kama mwakilishi wa Virginia katika bunge la katiba la Marekani mwaka 1787 akawa mwenyekiti wa mkutano huu uliokubali katiba ya Marekani.
Tarehe 4 Februari 1789 alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Marekani akirudishwa mwaka 1789. Baada ya kipindi chake cha pili alikataa kusimama tena akaunda hivyo utaratibu wa kwamba rais anaweza kurudishwa mara moja tu, hawezi kuendelea zaidi.
Remove ads
Mwisho na heshima baada ya kifo
Mwaka 1797 akarudi tena kwake shambani aliposimamia kilimo kilichoendeshwa na watumwa 390. Tarehe 14 Desemba 1799 alikufa kwake nyumbani. Kabla ya kuaga dunia aliamuru katika usia wake ya kwamba watumwa wake wote wapewe uhuru baada ya kifo chake yeye mwenyewe na mke wake.
Mji mkuu wa Marekani Washington, D.C. na jimbo la Washington vimepokea majina kutokana naye.
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads