Isaka wa Ninawi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Isaka wa Ninawi (kwa Kiaramu ܡܪܝ ܐܝܣܚܩ ܕܢܝܢܘ; kwa Kiarabu: إسحاق النينوي Ishak an-Naynuwī; kwa Kigiriki Ἰσαὰκ Σύρος, Isaac Syuros; kwa Kiingereza Isaac of Nineveh[1][2][3]; 613 hivi – 700 hivi) alikuwa mwanateolojia na askofu wa Kanisa la Asiria.

Ni maarufu hasa kwa maandishi yake juu ya maisha ya Kiroho. Yapo hadi leo katika lugha asili ya Kisiria na katika tafsiri za kale za Kigiriki na Kiarabu. Yametumiwa sana na Wakristo wa madhehebu mengine, hasa ya Mashariki [4].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, katika Kanisa lake na makanisa ya Waorthodoksi wa Mashariki na Waorthodoksi. Tarehe 9 Novemba 2024 Papa Fransisko alitangaza rasmi kwamba ataingizwa katika orodha ya Martyrologium Romanum [5].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Januari.
Remove ads
Maisha
Alizaliwa Beth Qatraye, kati ya Mesopotamia na Arabia (Qatar ?)[6][7][8].
Akiwa bado kijana sana alijiunga na monasteri akafanya bidii sana. Akitumia pia maktaba iliyokuwepo, alijipatia sifa upande wa teolojia akaanza kufundisha dini katika eneo lake asili.
Patriarki Georges alipotembelea eneo hilo katikati ya karne ya 7 ili kushiriki sinodi, alimfanya Isaka kuwa askofu wa Ninawi, Assyria, mbali sana, katika Mesopotamia ya Kaskazini.[9].
Majukumu hayo mapya hayakufaa tabia yake, hivyo baada ya miezi 5 alijiuzulu akarudi kusini katika upweke wa Mlima Matout. Huko aliishi miaka mingi akila mikate 3 tu kwa juma pamoja na mboga kidogo.
Hatimaye uzee na upofu vilimlazimisha kurudi monasterini. Huko Shabar alifariki na kuzikwa.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads