Kiukraini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kiukraini (kwa Kiukraini: українська (мова), ukrajins'ka mova) ni lugha ya Kislavoni cha Mashariki, mojawapo katika familia ya Lugha za Kihindi-Kiulaya.

Kiukraini ni lugha ya pili inayozungumzwa zaidi katika orodha ya lugha za Kislavoni. Kuna waongeaji milioni 37 wanaoongea lugha hiyo nchini Ukraini, ambapo ni lugha rasmi. Kwa wengi wa wenyeji wake lugha hiyo ni lugha mama. Kwa hesabu ya dunia nzima, kuna waongeaji wapatao milioni 47 wanaoongea lugha hiyo.
Remove ads
Alfabeti
Alfabeti ya Kiukraini kwa tafsiri ya maelezo kuelekea Kijerumani:
Remove ads
Kupiga marufuku lugha ya Kiukraini

Uharibifu wa Cossacks mwaka 1775 ulisababisha utumwa wa Waukraini na sera ya Urusishaji (kwa Kirusi: Русификация) - kupiga marufuku rasmi na uharibifu wa lugha na utamaduni wa Kiukraini na wakoloni wa Kirusi. Mfano wa kushangaza zaidi wa sera kama hiyo ni Amri ya Ems (kwa Kirusi: Эмский указ) na amri ya Piotr Valuev (kwa Kirusi: Валуевский циркуляр) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Dola la Urusi, hati hii kutoka mwaka 1863 ilisema kwamba lugha ya Kiukraini "haikuwepo, haipo na haiwezi kuwepo, na mtu yeyote ambaye hakubaliani na taarifa hii ni adui wa Urusi." [1][2]. Pia wakati wa Umoja wa Kisovyeti matumizi yake yalikuwa machache sana [3].
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads