Pambizo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Pambizo
Remove ads

Pambizo (vilevile kiungani, pambizoni, pembeni, kando ya mji, kiunga; kwa Kiingereza: suburb) ni makazi ya watu yaliyo pembezoni mwa mji au jiji na kitovu chake. Hukaliwa na watu wanaofanya kazi kwenye kitovu cha mji au kwenye mitaa ya viwanda. Si mjini kabisa wala si mashambani.

Thumb
Mapambizo huzunguka kitovu cha Kuala Lumpur, Malaysia
Thumb
Eneo la vibanda pale Soweto, pambizo la Johannesburg
Thumb
Maghorofa katika pambizo la Marzahn, Berlin, Ujerumani
Thumb
Mapambizo huzunguka kitovu cha Kontula, Helsinki, Finland

Zamani miji ya Dunia haikuwa mikubwa sana, isipokuwa miji mikuu katika madola makubwa yenye serikali thabiti. Tangu mapinduzi ya viwanda miji ilianza kukua na tangu mwaka 2008 zaidi ya nusu ya watu wote duniani huishi mjini[1].

Mifumo ya usafiri wa mjini inaruhusu watu kukaa mbali na mahali pa kazi na kusafiri kila siku baina ya nyumba na kazi.

Watu huamua kuishi kwenye mapambizo kwa sababu mbalimbali:

  • watu maskini hutafuta maeneo yasiyotumiwa wanapoweza kujenga vibanda vyao na hivyo kuanzisha pambizo la mtaa wa vibanda (slum)
  • watu wenye kipato kidogo hutafuta makazi ya kupanga kwa gharama isiyo juu yanayopatikana pale ambako bei ya ardhi ni nafuu
  • watu wenye hela hutafuta sehemu wanapoweza kujenga nyumba zao pamoja na nafasi ya bustani isiyopatikana tena mjini penyewe.

Kiutawala mapambizo yanaweza kuwa sehemu ya mji / jiji au kuwa nje yake. Hata hivyo kwa makusudi ya kusimamia usafiri, maji, maji machafu na takataka mara nyingi mamlaka za pamoja zimeundwa.

Remove ads

Tanbihi

Kujisomea

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads