Tarehe za maisha ya Yesu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Tarehe za maisha ya Yesu
Remove ads

Tarehe za maisha ya Yesu zinakadiriwa ili kuzidi kumfahamu Yesu kadiri ya historia.

Thumb
Picha takatifu ya Karne za Kati kutoka Urusi ikionyesha maisha ya Yesu.

Hii ni kwa sababu Injili na vitabu vingine juu yake havitaji kwa kawaida tarehe wala mwaka wa matukio vinavyoyasimulia.

Hata hivyo, vikitaja watu wanaojulikana na historia kwa njia nyingine (kwa mfano Kaisari Augusto na Kaisari Tiberi), au mambo mengine ya namna hiyo, inaweza kujua kwa kiasi kikubwa au kidogo mwaka au hata tarehe ya matukio hayo.[1][2]

Muhimu zaidi ni kukadiria Yesu alizaliwa akafariki lini.

Kuhusu kuzaliwa kwake, inajulikana kuwa kulitokea chini ya mfalme Herode Mkuu, aliyetawala hadi alipofariki mwaka 4 KK. Hivyo, wengi wanakubali kwamba Yesu alizaliwa kidogo kabla ya hapo, labda mwaka 6 KK[3][4][5][6]ingawa Denis Mdogo kwa kukosea alihesabu tofauti miaka 500 baadaye alipoona inafaa kugawa miaka yote ya historia katika makundi mawili, KK na BK.

Kuhusu kifo chake, kinashuhudiwa hata nje ya Biblia[7][8][9][10][11] kuwa kilitokea chini ya Ponsyo Pilato,[12][13][14] liwali wa Palestina kuanzia mwaka 26 hadi 36 BK.[15][16][17][18][19][19][16][20][21][22]Hivyo kifo cha Yesu kilitokea katika miaka hiyo.

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads