Yesu katika sanaa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Yesu katika sanaa
Remove ads

Yesu katika sanaa mbalimbali ameshika nafasi kubwa katika uchoraji, uchongaji, muziki n.k. vya milenia mbili tangu azaliwe.

Thumb
Sanamu ya marumaru maarufu kama Pietà ya Michelangelo Buonarroti inamuonyesha Yesu akiwa maiti mikononi mwa Bikira Maria.
Remove ads

Picha

Picha za Yesu Kristo zilitokeza mapema kwa namna nyingine jinsi Ukristo ulivyosogea mbali na Uyahudi uliopinga uchoraji wa Mungu na viumbe vyake kwa jumla.

Kwanza Yesu hakuchorwa, ila aliwakilishwa na ishara mbalimbali, kama vile samaki (kwa Kigiriki jina la samaki lilitumika kwa kuchukua kile herufi yake kama mwanzo wa neno zima lililomhusu: Yesu Kristo Mwana wa Mungu Mwokozi), Mchungaji mwema, Mfalme, Mwalimu.

Baadaye alianza kuchorwa kama kijana asiye na ndevu (hadi karne VI, lakini kuanzia karne IV hata akiwa na ndevu na nywele ndefu kama ilivyozoeleka zaidi baadaye.

Kutokana na mabishano ya karne VII na karne VIII kuhusu uhalali wa picha, katika Ukristo wa mashariki namna ya kumchora iliratibiwa.

Kumbe katika Ukristo wa magharibi Karne za Kati zilileta mwelekeo mpya, wa kibinadamu zaidi, hasa kwa kufuata mvuto wa imani kwa Yesu wa historia, yaani jinsi alivyoishi duniani.

Hatimaye katika Renaissance Kristo alianza kuchorwa kama kielelezo cha mtu mkamilifu hata upande wa sura.

Remove ads

Mifano ya michoro

Remove ads

Mifano ya sanamu

Mifano mingine

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads