Njombe (mji)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Njombe ni halmashauri ya mji wenye hadhi ya wilaya ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Njombe, nchini Tanzania, yenye postikodi namba 59100. Kabla ya kugawiwa eneo la Njombe lilikuwa sehemu ya Mkoa wa Iringa.

Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...

Misimbo ya posta ni 59101 (mjini, CBD) hadi 59117.

Njombe iko kwenye kimo cha mita 2,000 juu ya UB kwenye sehemu ya mashariki ya milima ya Kipengere, hivyo tabianchi ni baridi kiasi[1].

Mji uko takriban kilomita 200 kusini kwa Iringa na kilomita 150 upande wa kaskazini-mashariki kwa Mbeya.

Hadi mwaka 2012 kata za mji wa Njombe zilikuwa sehemu ya Wilaya ya Njombe ya awali; baadaye Njombe Mjini na Wilaya ya Njombe Vijijini zilitengwa kuwa halmashauri mbili za pekee.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 182,127 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya ya Njombe Mjini ilikuwa na wakazi wapatao 130,223 waishio humo. [3]

Wenyeji ni hasa Wabena. Lakini pia, kuna wingi wa watu wa makabila mengine kama Wakinga na Wapangwa.

Remove ads

Usafiri

Barabara ya lami kutoka Makambako kwenda Songea inapita mjini. [4]

Kituo cha karibu cha treni za TAZARA kipo Makambako. Pia kuna uwanja wa ndege eneo la Chaugingi.

Hakuna huduma ya ndege za abiria.

Dini

Njombe ni makao makuu ya Dayosisi ya Kusini KKKT ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania na pia ya Jimbo Katoliki la Njombe ya Kanisa Katoliki Tanzania. Kuna pia makanisa mengine na misikiti.

Eneo la Yakobi katika mji wa Njombe linatunza jina la kituo cha Wamisionari Walutheri Wajerumani waliofika mnamo mwaka 1899. Wakati wa Vita ya Majimaji kituo cha Yakobi kilishambuliwa na kikosi kilichoongozwa na chifu Mbeyela.[5]

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads