Mwokozi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Mwokozi katika teolojia ya Ukristo, ni sifa mojawapo ya Yesu kutokana na imani ya kwamba ndiye aliyetekeleza wokovu wa binadamu wote.

Ingawa Injili hazitumii jina hilo, Mtume Paulo alilieneza kupitia nyaraka zake kuhusiana na kifo chake msalabani.[1][2]
Hivyo Agano Jipya linamtaja Yesu Kristo kama Mwokozi mara 16, likisisitiza kuwa ameokoa wote.[3]
Waraka wa kwanza wa Yohane unamtaja kama "kipatanisho cha dhambi zetu, tena si cha dhambi zetu tu, bali cha dhambi za ulimwengu" (1 Yohane 2:2).[4]
Mbali ya Yesu, Agano Jipya linatumia jina hilo kwa Mungu tu (mara 8), wakati Agano la Kale linaita watu mbalimbali kwa jina hilo, kwa sababu ya kuokoa mtu mmoja, wachache au wengi kutoka matatizo mbalimbali.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads